
imekua ni jambo la kawaida kwa koffi olomide kujigamba kila apatapo nafasi, sasa kaja mpya akidai yeye ndo bosi wa muziki kongo na hakuna kama yeye! ilikua ni wakati akijibu shutuma kwa nini wanamuziki hawadumu katika bendi yake, akadai yeye ni mwalimu anawapika na kuwaacha wakajitafutie, akawatolea mifano kama fally, fere gola na wengine kibao.
1 comment:
Well! Tofauti kati ya Mwanamuziki Koffi na waimbaji tunaowasikia wakijitamba nyumbani ni kuwa maneno ya Koffi husindikizwa na matendo. Unaweza kukumbuka alipokimbiwa na kundi karibu zima akaunda vijana na kutoa Attentat ambayo haikuwa albamu kali zaidi kwake, lakini haikuwa mbali kwa ubora ukilinganisha na muda alioitengeneza. Lakini waimbaji wetu kila mwaka watasema "sasa nakuja kivingine na kaeni mkao wa kula" nasi mashabiki tunajishindisha njaa tukiwa mkao wa kula lakini wakija kupakua, hata popcorn zinashibisha. Inasikitisha.
Kwa hiyo nadhani Koffi licha ya kujitamba kuliko anavyostahili, lakini ana uwezo kiasi katika hayo ayasemayo na pengine kujitamba huko ndiko kunakomfanya ajiandae vema akijua kuwa ana"deni" kwa mashabiki wake.
Blessings
Post a Comment