Thursday, November 19, 2009

TIKISIKA NA DECEMBER YA URODA

ni uroda wa aia yake december hii ndani ya uwanja wa samora, picha hii ni show ya MTIKISIKO mwaka jana na sasa ni tarehe 6 december, na show ina mabadiliko makubwa, so wadau niko bize kidogo na maandalizi hivyo ntakuwa nikija kuwasalimu na kuwapa maendeleo ya uroda wa december, msijali.

Tuesday, November 17, 2009

YES! NI YOUSSOU N'DOUR! IN DAR!


Monday, November 16, 2009

KWA JOHN MWAIPOPO, NA WADAU WENGINE

hiki ndo kile alichoongea john mwaipopo kuwa mheshimiwa alivua shati stars iliposhinda, hapa tuliwagonga burkina faso na mapokezi ndo yalikua hivi,

MBUNGE ANAPOLISAKATA TWANGA PEPETA!

si ajabu katika hafla mbalimbali kuwaona viongozi wetu wakiserebuka na wanamuziki wetu, lakini utamu wa hii ni kwamba mh mohamed dewji mbunge wa singida mjini (ccm) aliamua kupanda jukwaani kabisa na kwenda sambamba na wanenguaji wa bendi ya twanga pepeta, halafu hebu cheki hilo snepu ni kama braza mzoefu vile? kama vipi wabunge waanzishe bendi yao jamani tupate uhondo.

Friday, November 13, 2009

MISHEMISHE 24/7

jamaa ni kama analala vyumbani mwa ma star wa ulimwengu, ukikinukisha tu analo, anaitwa JULIAN ISHUNGISA jamaa ana mishemishe masaa 24 kifupi halali nakupa siri ukimta kampate hapa http://twentyfoursevenmishemishe.blogspot.com/

Wednesday, November 11, 2009

MIAKA 22 YA QUARTIER LATIN FERRE, FALLY NDANI!

sio ndoto wala hadithi za kufikirika MOPAO KOFFI OLOMIDE katika sherehe za miaka 22 ya L’orchestre Quartier Latin International amedhamiria kwaalika wanamuziki wote waliopitia katika band yake. tukio hilo litafanyika jumamosi ya november 28 ndani ya Grand hotel jijini kinshasa. katika list ya walioalikwa majina kama fally ipupa na ferre golla yapo kwenye v.i.p list. haya bwana huyo ndio koffi bwana, tusubiri kuona nini kitatokea na kama ada nitawapa vipande hapahapa kunako VIVA. papaa joe mutu ya zenji upoooo.

LIBENEKE LA ZIARA YA RAS NAS!

Ile ziara ya mwanamuziki Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi katika miji sita ya Norway karibu inamalizika. Hapa ni kwenye ukumbi wa MS Innvik, Oslo, ambapo Ras Nas na kikosi chake waliwasha moto mkali usiku wa Halloween; Jumamosi iliyopita. Hivi sasa Ras Nas amejipanga kufyatua CD ya muziki na mashairi "Double Focus". Mashairi yanatoka kwenye kitabu ambacho Nasibu aliandika mwaka 1989 pamoja na shairi moja la Shabaan Roberts “Titi la Mama”. Kwa hiyo hivi sasa kaa chonjo!picha na habari kwa hisani ya Wadau wa Kongoi Productions http://www.kongoi.com/

Tuesday, November 10, 2009

POLE SANA DADA JACKLINE CHARLES!

nilijiuliza kwa muda alipo mdogo wangu mpenzi jackline charles na leo kanambia alipata mkasa wa kuvamiwa na majambazi, na kujeruhiwa. pole sana dada, nashukuru waendelea vema, MUNGU akujaalie nafuu urejee kazini na bloguni pia, POLE SANA MDAU. msalimie hapa http://jacklinecharles.blogspot.com/

TUKUNYEMA MPAKA CHINI,,,,,,,,,,,,,,,,,,

tume ya maadili inaposhangilia namna isiyofurahisha ya uchezaji kwa madensa wao, lakini hivi sasa congo uvaaji na staili ya uchezaji ni mjadala mkubwa, hapa kwetu basata waliwahi kutishia kuzifungia bendi za dansi ambazo wanenguaji wake wanavaa bila kuzingatia maadili, haya ngoja tuone nini kitafuata katika mjadala huu.

Monday, November 9, 2009

FALLY NA OLIVIA FULL MALAVIE DAVIE!


cheki jinsi fally ipupa anavyotesha na olivia wa g unit, nlipopata chance ya kukaa nae alipokuja tanzania kizungu hakipandi na kiswahili ni mgogoro mwingine, hapo ni french na lingala, sasa sijui mawasiliano hapo yakoje mie mgeni wadau.

KOFFI HUYOO TENA AMEKINUKISHA!

ilikua ni kama hadithi na sasa mambo yanamweneda kombo mopao koffi oliomide, jamaa anakabiliwa na mashitaka ya ubakaji na huenda akahukumiwa na mahakama ya ufaransa ambako kesi hiyo inaunguruma. kwa mujibu wa taarifa miaka miwili iliyopita akiwa katika ziara ya kimuziki nchini huko alikua na wacheza show wake wakiwemo mabiti 4 wenye umri kati ya miaka 14 na 17 na kwa mujibu wa sheria hilo ni kinyume cha sheria, koffi anadaiwa kuwafungia wasichana hao ndani chini ya ulinzi mkali na kazi yao ni kumrisha kimapenzi anapowahitaji, haya kama mjuavyo hapa viva hapakauki mambo endelea kuwa nami ntakupa kitakachojiri.

Monday, November 2, 2009

MKWALA WA SOLEIL WANGA STUDIO,,,,,,,,,

mwanamuziki soleil wanga akiwa na wenzie mamadou na koulibaly katika upishi wa album yake ya"APRÈS TOI", soleil amejinadi kuwa album yake yaja na ubora wa kiwango cha kimataifa ili asiwaangushe watu wake.

NYOTA NDOGO: MUZIKI MPAKA UTANGAZAJI!

msanii toka mombasa kenya Mwanaisha Abdalla a.k.a Nyota Ndogo yu mbioni kuanza kazi ya utangazaji hivi karibuni. nyota anawindwa na kituo cha Baraka FM ili ajiunge na timu hiyo. mapaparazi walimfumania nyota katika jengo la Cannon Towers zilipo ofisi za Baraka FM ambako yasemekana anapata mafunzo ya RADIO. taarifa zimezidi kumwagika kuwa mkali huyo atakuwa akiendesha kipindi kimoja mwisho wa wiki kitakachoanza kuruka mwishoni mwa mwaka. NZULA MAKOSI ndiye mwalimu wa nyota kuendesha vifaa vya studio. "ni kweli napata mafunzo hayo, lakini mmepata wapi taarifa hizo?" alihoji nyota ndogo.

Saturday, October 31, 2009

RAHA JIPE MWENYEWE!


Friday, October 30, 2009

KINSHASA HAPATOSHI THIS DECEMBER! UNABISHA?

umezoea kuskia wanamuziki toka afrika wakienda kupiga show ulaya, na ni wachache wao huja kwetu, ni tofauti kwa wakazi wa kinshasa, mwenyewe cheki halafu mwaga komenti.

Thursday, October 29, 2009

TECHNO MALEWA YA WERRASON HAISHIKIKI!

kama utani vile lakini ndio mkanda kamili, album ya ngiama makanda werason ya techno malewa huko sokoni tayari imegonga nakala zaidi ya 125 000 na bado yagombewa kama msosi kwa wenye dhiki ya chakula, tusubiri tuone kama itavunja rekodi.

Wednesday, October 28, 2009

WATOTO WA KOFFI WAKO SOKONI KWA FUJO!

vijana walioitumikia kwa mafanikio makubwa "Quartier Latin Internationale" ya KOFFI OLOMIDE, soleil wanga, fally ipupa, na ferre gola ambao wote sasa wanafanya kazi kama wasanii wa kujitegemea na tayari album zao ziko sokoni. haya wadau pedeshee ndama, papaa musofe"chuma cha reli", big producer maghambo, abdull tall, bila kumsahau pius mikongoti nipeni data nani mkali hapa.


Tuesday, October 27, 2009

TUKUMBUKE ENZI ZA FAMILIA YA "MAKOMA"

hawa ni wanamuziki wa makoma majina yao ni nathalie, penganie, annie, martin, na tutala duma na rafiki wa familia patrick naomba story zao wadau, enzi zile za "butu na moyi"

Monday, October 26, 2009

KOFFI OLOMIDE HAISHI VITUKO!

mwaka 2002 koffi olomide na papa wemba walitoa album ya "wake up" na hivi karibuni papa wemba alitoa malalamiko kuwa koffi hakufanya sawa katika mapato ya album hiyo sasa limeibuka jipya, aliyekuwa mzalishaji mkuu wa album hiyo coco rubenga katika mtandao wa intaneti ametangaza kuwa anamdai koffi kiasi cha $ 120,000 ambazo ni sawa na euro 80,000 ambazo alifanya kazi katika album hiyo.
kwa upande wake papa wemba ameomba radhi na kuahidi kufanya kile kinachomstahili, lakini koffi amedharau hata amri ya mahakama na hivyo kuzua mjadala mkubwa, jamaa haishi vituko sasa tungoje itakuaje.

MWANA BARAZA MWINGINE HUYU HAPA!

ulimwengu wa teknohama unakua kila siku na hata katika ulimwengu wa tatu mwendo kasi unaongezeka pia, hapa mzee wa viva afrika nikila snepu na mdau agness anderson ambaye naye kagonga hodi kwenye ulimwengu wa kublogisha, karibu sana mdau, swali ni kwamba utashika bomba? manake safari ndefu hii! karibu barazani utupe utamu. mapate hapa http://www.kiduchu.blogspot.com/