Monday, October 26, 2009

KOFFI OLOMIDE HAISHI VITUKO!

mwaka 2002 koffi olomide na papa wemba walitoa album ya "wake up" na hivi karibuni papa wemba alitoa malalamiko kuwa koffi hakufanya sawa katika mapato ya album hiyo sasa limeibuka jipya, aliyekuwa mzalishaji mkuu wa album hiyo coco rubenga katika mtandao wa intaneti ametangaza kuwa anamdai koffi kiasi cha $ 120,000 ambazo ni sawa na euro 80,000 ambazo alifanya kazi katika album hiyo.
kwa upande wake papa wemba ameomba radhi na kuahidi kufanya kile kinachomstahili, lakini koffi amedharau hata amri ya mahakama na hivyo kuzua mjadala mkubwa, jamaa haishi vituko sasa tungoje itakuaje.

1 comment:

chib said...

Waliokuwa wanadai huyu jamaa huwa anavuta sigara ya pingili labda hawakukosea!!