Monday, November 2, 2009

NYOTA NDOGO: MUZIKI MPAKA UTANGAZAJI!

msanii toka mombasa kenya Mwanaisha Abdalla a.k.a Nyota Ndogo yu mbioni kuanza kazi ya utangazaji hivi karibuni. nyota anawindwa na kituo cha Baraka FM ili ajiunge na timu hiyo. mapaparazi walimfumania nyota katika jengo la Cannon Towers zilipo ofisi za Baraka FM ambako yasemekana anapata mafunzo ya RADIO. taarifa zimezidi kumwagika kuwa mkali huyo atakuwa akiendesha kipindi kimoja mwisho wa wiki kitakachoanza kuruka mwishoni mwa mwaka. NZULA MAKOSI ndiye mwalimu wa nyota kuendesha vifaa vya studio. "ni kweli napata mafunzo hayo, lakini mmepata wapi taarifa hizo?" alihoji nyota ndogo.

1 comment:

XTRA COVER. said...

Kweli kaka aliedhamiria sarafi huwa hachoki kusafiri.

Binafsi ninampongeza dada yangu kwa kuingia katika fani ambayo inaheshimiwa kwa sasa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.

ORIENTE dada NYOTA NDOGO.