Tuesday, July 7, 2009

NI KWELI WANAMUZIKI MALAYA AU UZUSHI TU.

eti wadau ile hoja ya wanamuziki ni malaya ina ukweli kiasi gani? nimelazimika kuleta waraka huu baada ya kuzuka ubishi mkubwa ofisini kwangu leo, sasa tujadili kwa upana na wenye mifano hai itoeni bila hofu. hapo juu ni mwanamuziki wa msondo papa upanga akipagawa na kiuno cha shabiki wake na chini ni roman a.k.a romario akidatishwa na mauno ya densa wake, kazi kwenu wadau.


1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Hakuna ukweli kuwa wanamuziki ni "wahuni" (samahani ntatumia hili neno badala ya hilo, lakini nadhani maana zakaribiana). Na nasema hivi kwa kuwa MUZIKI kama muziki ni kazi, ni wito, ni uelimishaji, ni kioo katika jamii kama utatumika unavyostahili. Linalotuharibia hapa ni kuwa wapo waliovamia kazi, wito na uelimishaji wa wenzao na matokeo yao wanakosa ama kushindwa kufuata maadili na mikondo halisi ya kazi. Matokeo yake ni kudhalilisha fani nzuri na yenye nafasi kubwa ya kuielimisha jamii. Na uvamizi huu (ambao umeingia mpaka kwenye siasa na kuifanya ionekane kama njia ya kuiibia na kuidanganya huku ukiikandamiza jamii) ndio unaojenga picha mbaya kwa jamii kuhusu MUZIKI. Wasio na wito wala kipaji hulazimisha kwa kufanya mambo yanayoleteleza kashfa mbalimbali. Wataanza kutunga nyimbo za kuleta mabishano, magomvi na majibizano ili wapate "attention" na pia kucheza isivyo ili kuvutia watu kwa kuwa kwa kufanya hivyo ndio wataweza kupata watu wa kuwakodolea macho na hata kuwatunza. Kwa hiyo naamini na NAJUA kuwa muziki na wanamuziki si (ama niseme hawatakiwa kuwa) wahuni, na wanaonekana hivyo kutokana na wasio na vipaji na wito "kuvamia viwanja vyao". Hawa wanaofanya hivi niliwaandika kwenye makala inayopatikana http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/wasanii-wetu-wanavyokuwa-wasivyo.html