Wednesday, October 7, 2009

RAHA YA MCHEMSHO BAADA YA KAZI!

dada yasinta, kaka mubelwa na wadau wenzangu wote mlionimis kwa muda nimepeokea salamu zenu na nimeona ni vema niwaeleze jambo, kwa takriban wiki moja na siku mbili nlikua na kazi za nje (field work) hivyo mwili ulichoka barabara kwa jua la mchana kutwa na vumbi lililonitandika vizuri, hivyo ndo nimerejea kwenye dawati na kama mwonavyo najenga mwili kwa mchemsho matata, hapo ni minyama, mindizi, miviazi, minjegere, micaroti, mipilipili hoho katika chombo kimoja. najua mmepata kajiharufu kazuri katika hii picha.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli ulimisiwa kweli na tunashukuru sana umerudi unajua sisi sasa ni wanandugu tena mapachamapacha akipotea mmoja mmoja hana raha. Huo mchemsho kaka nimeutamani kweli ila basi tu. Shukrani kwa kutujuza wapi ulikuwa.

Mzee wa Changamoto said...

Ni faraja kukuona tena. Na zaidi kukuona ukiwa bukheri wa afya. Hilo kwetu ni Baraka kubwa. Basi salimia wote wa "kipande ya Iringa". Kina Shaban, Allen na wa Anga la Michezo. Kina Dadaa wa Mbeya Fm na hapo kwenu. Mko wengi mtandaoni na mnastahili kuheshimika kwa hilo.
Twawapenda na kuwakumbuka huku TUKIWAOMBEA.
Blessings

Anonymous said...

Gape! imagine untoka kazini na njaaaaa then unakuja home wakuta madikodiko kama hayo lazma udenda udondoke. Hebu furahia huu msosi mana nakumbuka siku amabzo ilikua kula kwa kiboko.Nakukosa wangu, its great to see you doing so well my dear!!!
Baby Luv