Saturday, October 19, 2013

FALLY NA UJUMBE WA AMANI MASHARIKI MWA CONGO!!


Mwanamuziki mwenye mafanikio ya juu kwa sasa nchini Congo aishiye ufaransa  FALLY IPUPA anatarajiwa kuwasili kinshasa kwa onesho maalum  kama balozi wa amani huko mashariki mwa kinshasa.

Fally anatarajiwa kuandamana na wachezaji kadhaa wa soka wa congo wanaocheza barani uropa kwa lengo la kufanya harambee huko goma, eneo ambalo limetawaliwa na mapigano kwa muda mrefu sasa.
Fally pia atatumia ziara hiyo kutambulisha album yake mpya aliyoipa jina la " Power kosa, leka"
 baada ya onesho la Goma tarehe 24 fally ataunguruma Bukavu tarehe 27 octoba.
haya sasa mwana wa afrika huyo tena  akiibeba bendera ya amani Congo.