Sunday, October 20, 2013

JULIANA KANYOMOZI AREJEA JUKWAANI BAADA YA MIAKA SITA!!

Msanii mahiri wa Uganda mwenye sauti mithili ya kinanda JULIANA KANYOMOZI amewaacha watu hoi usiku wa kuamkia jumamosi katika ukumbi wa victoria, ndani ya serena hotel, baada ya kuwakata kiu ya miaka sita ya kumsubiri ndege mnana huyo kupanda jukwaani kutumbuiza.
JULIANA alipiga nyimbo zake kali zote za zamani na mpya huku akipewa kampani na wasanii na mastaa kibao.
pia jaji huyo wa shindano la kusaka vipaji la TUSKER PROJECT FAME, aliwashukuru wapenzi wa muziki wake kwa kuja kwa wingi kwenye onyesho lake!! kutoka VIVA AFRIKA twakukaribisha tena jamvini JULIANA KANYOMOZI!!