Wednesday, September 23, 2009

OLIVER MUTUKUDZI KUSAIDIA WANAWAKE NAIROBI

Mwanamuziki mahiri barani afrika wa nchini Zimbabwe oliver mutukudzi anatarajiwa kuwasili nchini Kenya muda wowote toka sasa kwa ajili ya tamasha lililolenga kuchangisha fedha kwa hospitali ya wanawake ya Nairobi.
Mutukudzi anatarajiwa kuongozana na wanamuziki wake saba katika ziara hiyo na kuangusha show bab kubwa katika ukumbiwa Nairobi Arboretum hapo ijumaa ya tarehe 25 setember.
“Nairobi women’s hospital” ina kitengo maalum cha “Gender Violence Recovery Centre (GVRC)” ambacho tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 kimesaidia watu 14,000 toka katika manyanyaso ya kijinsia.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Napenda kuwatakia mafanikio mema na pia natanguliza shukrani kwa mwanamuziki Oliver kwa kuwa na moyo wa kupenda kuwasaidia wanawake. Viva Oliver, na viva Afrika.