Thursday, July 11, 2019

TWANGA PEPETA NA KIBODABODA CHAO!!

Bado muziki wa dansi bongo haujafa na wanamuziki wanafanya jitihada na kuupigania!! hapa twanga pepeta wakijifua kwa style mpya wanaiita KIBODABODA!!! usipange kuikosa.

Wednesday, July 10, 2019


habari wadau wangu wa VIVA AFRIKA, baada ya kunimiss kwa kitambo hivi sasa nimerejea!!! endelea kupata burudani ya kiwango toka hapa...

ALLY CHOKI BADO AIOTA EXTRA BONGO!!

Mwanamuziki nguli wa dansi nchini ALLY CHOKI bado anaiota bendi yake ya EXTRA BONGO na ameapa kuirejesha tena mapema mwakani. choki kwa sasa yuko jijini mwanza akifanya kazi na bendi ya super kamanyola kwa mkataba wa miezi sita. baki hapa hapa VIVANI kwa mastori matamu ya muziki wa dansi.

Saturday, April 19, 2014

RADIO NA WEASEL HAOO TUZO ZA BET!!

The Dybamic duo Weasel and Radio had previously been nominated for the 2013 BET Awards
Kwa mara nyingine tena wasanii toka uganda Weasel na Radio  wameinua bendera ya nchi yao juu kwa kupendekezwa katika katika tuzo za  BET, wimbo uliowaingiza kwenye mtanange huo ni kiboko changu katika kundi la wimbo bora wa kushirikishwa ambao wamemshirikisha msanii amani toka kenya.
Kiboko Changu song  utashindana na nyimbo zingine kali kama  Number One wa  Diamond na Davido, Happiness wa Mafikizolo na  May D, Slow Down wa  R2bees na Wizkid na Y-tjukutja wa Uhuru alomshirikisha DJ Buckz, Oskido, Professor na Yuri Da Cunha

KOFFI ACHAFUKWA, SASA KUCHAJI ILI KUPATA MAHOJIANO NAYE!!

Ndio ni kweli koffie amefikia maamuzi hayo baada ya kukerwa na waandishi wa habari ambao wanaandika habari kwa makusudi ya upotoshaji na kuharibu hali ya hewa katika bendi yake na kwa familia yake pia. alisema sasa atakuwa anachaji pesa kwa kila mtu atakaye mahojiano naye kama wafanyavyo ulaya na marekani.

Sunday, October 20, 2013

JULIANA KANYOMOZI AREJEA JUKWAANI BAADA YA MIAKA SITA!!

Msanii mahiri wa Uganda mwenye sauti mithili ya kinanda JULIANA KANYOMOZI amewaacha watu hoi usiku wa kuamkia jumamosi katika ukumbi wa victoria, ndani ya serena hotel, baada ya kuwakata kiu ya miaka sita ya kumsubiri ndege mnana huyo kupanda jukwaani kutumbuiza.
JULIANA alipiga nyimbo zake kali zote za zamani na mpya huku akipewa kampani na wasanii na mastaa kibao.
pia jaji huyo wa shindano la kusaka vipaji la TUSKER PROJECT FAME, aliwashukuru wapenzi wa muziki wake kwa kuja kwa wingi kwenye onyesho lake!! kutoka VIVA AFRIKA twakukaribisha tena jamvini JULIANA KANYOMOZI!!

Saturday, October 19, 2013

FALLY NA UJUMBE WA AMANI MASHARIKI MWA CONGO!!


Mwanamuziki mwenye mafanikio ya juu kwa sasa nchini Congo aishiye ufaransa  FALLY IPUPA anatarajiwa kuwasili kinshasa kwa onesho maalum  kama balozi wa amani huko mashariki mwa kinshasa.

Fally anatarajiwa kuandamana na wachezaji kadhaa wa soka wa congo wanaocheza barani uropa kwa lengo la kufanya harambee huko goma, eneo ambalo limetawaliwa na mapigano kwa muda mrefu sasa.
Fally pia atatumia ziara hiyo kutambulisha album yake mpya aliyoipa jina la " Power kosa, leka"
 baada ya onesho la Goma tarehe 24 fally ataunguruma Bukavu tarehe 27 octoba.
haya sasa mwana wa afrika huyo tena  akiibeba bendera ya amani Congo.


Wednesday, October 16, 2013

MIAKA 24 YA KUMBUKUMBU YA FRANCO CONGO KIMYA KIMYA!!

Tarehe 12 mwezi huu ilikua kumbukumbu ya gwiji na nguli wa muziki wa rhumba nchini congo FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI lakini ilipita kimyakimya hali ilofanya wadau kujiuliza kama mchango wake kwenye muziki wa congo umesahaulika??

Sunday, October 13, 2013

BEBE COOL AMKERA MBUNGE BETTY NAMBOOZE UGANDA!

Mwanamuziki wa uganda bebe cool amejikuta kwenye wakati mgumu kama jaji wa onesho la kusaka vipaji kwenye runinga ya NTV baada ya mbunge wa mukoro kaskazini BETTY NAMBOOZE kumbwatukia kwenye mtandao kwa madai kuwa amekuwa jaji mbaya na hawapi vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao na anatumia maneno makali mno ya kuwakatisha tamaa watoto hao ambao wanajitahidi kutaka kutoka kimaisha kupitia muziki.

Saturday, October 12, 2013

NI JB MPIANA ZENITH TENA!

Hatimaye ule utata wa kama onyesho litafanyika umetatuliwa na waandaaji wa onyesho hilo huku Taasisi ya uendelezaji utamaduni na wamiliki wa ukumbi maarufu wa Zenith wamethibitisha onyesho hilo kwa kuweka tangazo la onyesho hilo linalotazamiwa kufanyika Dec 21.
JB Mpiana alikuwa nchini Ufaransa mwezi September na inasemwa kwenye ndege walikuwa na hasimu wake Werasson Ngiama Makanda ambaye pia amesaini kupiga onyesho kwenye ukumbi huo huo bado tarehe haijapangwa.
Swali linabaki je onyesho litafanyika bila fujo au kipingamizi kutoka kwa Bana Congo???

Monday, October 7, 2013

VIPI HAPA FALLY VS LADY JAY DEE WAKIPIGA COLLABO?

Naam ni mwana wa congo anayetesa vilivyo akiwa na mwana wa bongo mwenye mafanikio lukuki walipokutana jijini nairobi hivi karibuni, vp wakitoa collabo!! skilizia papa VIVA AFRIKA

Sunday, September 15, 2013

FALLY SASA KWENDA SAWA NA R KELLY!!


Mwana wa afrika ambaye alitabiriwa makubwa alipoamua kuwa mwanamuziki wa kujitegemea sasa anazidi kutanua mbawa zake, ni hivi juzi tu fally ipupa amemaliza kazi ya kurecodi wimbo wake mpya uendao kwa jina la POWER akiwa amemshirikisha gwiji wa miondoko ya R & B R, kelly! Fally ambaye yuko busy mno kwa ziara za kikazi duniani kote, anatarajia kuitambulisha albam yake hiyo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Monday, June 17, 2013

WERASSON USO KWA USO NA JB MPIANA, PATAMU HAPO!!


Live bila chenga kutoka kinshasa habari zinanyetisha kuwa yaandaliwa show moja kubwa na maalum itakayowakutanisha katika jukwaa moja magwiji wa wenge musica bcbg(jb mpiana) na wenge musica meison merre (werasson), tarehe ni 26 ya june na eneo la tukio ni katika uwanja wa stde des martyrs. waswahili husema mafahari wawili hawakai zizi moja, kitakachojiri ntakujuza papa hapa kunako viva.

Wednesday, June 5, 2013

FERE GOLA KUITAMBULISHA `BOITE NOIRE` KINSHASA!!


Sasa imethibitika rasmi kuwa kabla ya mwisho wa mwezi wa sita nguli mwingine toka congo FERE GOLA nae ataipakua album yake ya tatu tangu awe mwanamuziki wa kujitegemea, akifafanua kiongozi wa bendi hiyo ya jet set inayomilikiwa na ferre  amesema album hyo inakwenda kwa jina la `boite noire` ikimaanisha kasha jeusi imetayarishwa chini ya kampuni ya diego music chini ufaransa.ferre anatarajiwa kinshasa wakati wowote toka sasa kwa ajili ya uzinduzi wakati kiongozi wa bendi yake vasco mabiala yeye anasimamia zoezi la uzalishji wa cd na dvd za album hiyo. haya kama kawa wapenzi wa rhumba tuusubirie mzigo huo wa ferre gola a.k.a shetani!!!! papa mikongoti upooooo

Thursday, May 23, 2013

KOFFIE OLOMIDE AIBWATUKIA TENA SERIKALI YA CONGO!!

wanamwita quadra koraman, ambaye ametoa dukuduku lake la moyoni kwa seikali yake akiwakilisha wasaii wengine wengi wa congo ambao huvuna pesa nyngi katika ziara zao nje ya congo, koffie anasema kwanza wanalazimika kulipa kodi nyingi wanapotaka kusafiri nje ikiwemo na kulipia vibali katika uwanja wa ndege wa Ndjili, kodi hizo zamnufaisha nani? alihoji mopao! pia aliitaka serikali iwasaidie wanamuziki wa congo kujenga studio ya kisasa ya kuzalisha muziki wao ili kuwaepusha na gharama za kwenda ulaya kwa ajili ya kazi hiyo kitu kinachowagharimu mno, koffie alikuwa akizugumza katika kipindi cha `info 7` kilichorushwa moja kwa moja na congoweb TV wakitangaza kutoka kinshasa ambapo pia koffie alitangaza nia yake kujitupa kwenye siasa.

Sunday, May 19, 2013

TRACE MUSIC AWARDS 2013, FALLY ANG`ARA

Katika kile kionekanacho bado mvua ya mafanikio bado yamnyeshea FALLY IPUPA tayari ametwaa tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume kwenye tuzo za TRACE 2013, huku akiwa jikoni kwa upishi wa album yake mpya chni ya kampuni ya universal music.haya tu0ngoje fally baada ya bicarbonate anakujaje 2013?

Thursday, May 16, 2013

WAZEKWA YU TAYARI KUWALETA ADAM NA EVA!!

Hasimu mkubwa wa koffie olomide felix wazekwa amegonga vichwa vya habari baada ya kutoa picha hii akimaanisha yuko tayari kuingia sokoni ambako tayari koffie anapeleka puta roho za wapenda burudani kwa mkwaju wake wa abracadabra! haya sasa adam na eva hiyoooo, tuama hapahapa VIVA utajua kitakachoendelea.

Sunday, May 12, 2013

UZINDUZI WA RISASI KIDOLE WAFANA BUSINESS PARK!!

Naam, hatimaye naye Charlz baba ameingia rasmi katika kundi la marais wa bendi za dansi hapa bongo akiliongoza barabara kundi la mashujaa musica! hapa ni katika uzinduzi wa album ya mashujaa rais wa FM ACADEMIA  nyoshi el sadat akimvisha medali charlz baba! unaambiwa business park ilipendeza kwa show tam na kali toka kwa bendi kali. hongera charls baba kuiongoza vema mashujaa kuonesha ushujaa na kizindua album yenu ya risasi kidole.

Wednesday, May 8, 2013

NGWASUMA KUUNGURUMA NEW MAISHA CLUB!!

katika kile kionekanacho kama muziki wa dansi unarudisha hadhi yake ilopigwa kumbo miaka ya hivi karibuni, tayari matukio ya kiburudani yanazidi kuongezeka, haya sasa wapenzi na washabiki wa FM ACADEMIA habari yajieleza hapo, mzee wa viva siongezi neno!!