maji hufuata mkondo ila mkondo huu si mchezo, binti kajaaliwa vipaji lukuki nae anavitendea haki, toka ulimbwende, muziki hadi filamu TABIA BATAMWANYA anadhihirisha kuwa yeye si bahati mbaya kuzaliwa kwenye familia ya sanaa.kwa sasa anakimbiza na wakali wengine katika bendi ya k mondo sound chini ya mtaalam richard mangustino, sasa fuata nyuki ule asali.
Sunday, May 5, 2013
MASHUJAA KUTAMBULISHA RISASI KIDOLE MEI 11
Haya sasa wana afrika wenzangu shughuli ndo hiyo inaalika washughulikaji, si shindano wala mpambano, ila hakika patachimbika, wakati mashujaa watakapopakua RISASI KIDOLE pale business park may 11. huku ngwasuma kule kibega, twenzetu wana afrika tuwape sapoti mashujaa wanapotoka kishujaa.
Saturday, May 4, 2013
NANI KASEMA BANZA KAISHA!!
Ramadhani masanja al maarufu kama banza stone akiwajibika jukwaani kumpa sapoti rapa kaba tano kuonesha bado anadai
na utamu wa muziki kama hivi totoo ze bingwa na mtu mzima banza stone wanapokukutana jukwaa moja
na utamu wa muziki kama hivi totoo ze bingwa na mtu mzima banza stone wanapokukutana jukwaa moja
Friday, April 26, 2013
FALLY IPUPA AILEZA UJIO WAKE WA 2013!!
Mwanamuziki wa congo asoisha vituko na mkali wa mavokali na vibweka stejini fally ipupa juzi amefunguka na kueleza mikakati yake ya mwaka 2013 akiwa chini ya kampuni inayosimamia kazi zake ya univesal music kuwa itakuwa moto! fally aliyasema hayo wakati akiongea na television ya taifa ya congo.
MAPACHA KUINADI YARABI NAFSI MIKOANI!!
Baada ya kuitambulisha rasmi albam yao ya pili ya YARABI NAFSI jijini dar bendi ya mapacha watatu sasa wako mbioni kufanya ziara ndefu mikoani ili kuwapa raha na ladha wapenzi na mashabiki wao wakiwa na sura mpya baada ya kalala jr kurejea twanga pepeta, ziara hiyo inatarajiwa kuanza jijini dodoma tar 1may na kuendelea mjini morogoro tar 10 kisha mikoa mingine itatangazwa.
MIZUKA YA DANSI NA MBWEMBWE JUKWAANI!!
Muzuki una mbwembwe jamani balaa, tazama wanenguaji wa bendi ya EXTRA BONGO next level wakiwa kazini huku wakicheza style ya kushika *chakula ya mtoto* unaambiwa hapa kazi tu.
Mkurugenzi wa bendi ya EXTRA BONGO next level kamarade ally choki nae hakuwa nyuma kumpagawisha na kumpa mizuka mpiga solo wake ephraim joshua ili mabo yaende muswano.
Mkurugenzi wa bendi ya EXTRA BONGO next level kamarade ally choki nae hakuwa nyuma kumpagawisha na kumpa mizuka mpiga solo wake ephraim joshua ili mabo yaende muswano.
KOCHA WA DUNIA JUKWAANI TENA!!
Prince muumin mwinjuma bado king`ang`a nizi kwenye libeneke la muziki wa dansi, baada ya safari ndefu sasa analiongoza kundi jipya la VICTORIA SOUND akiwa na majina mahiri kama waziri sonyo na damu changa pia! haya sasa wapenzi wa muziki wa dansi, na maneno ya vijembe ya muumini kazi kwenu.
NIMEWAMISS WADAU WANGU WA IRINGA!
Mzee wa viva niko na mtu mzima allen sean phillips (aliyekaa) kwenye maonyesho ya utalii uwanja wa samora iringa!
HONGERA AGGY a.k.a KIDUCHU
Thursday, April 18, 2013
BURIANI FATMA BINT BARAKA (Bi Kidude)
Nembo ya ukweli ya muziki wa taarabu inayotambulisha tanzania, bendera iliyopepea kwa zaidi ya karne moja bila kupoteza thamani yake, kinywa kisichokauka maneno na tungo zitakazodumu daima! buriani Fatma bint Baraka almaarufu kama bi kidude!
Monday, December 5, 2011
HALI YANGU YAENDELEA VEMA!
Thursday, December 1, 2011
PATCHO MWAMBA "TAJIRI" MUZIKI HADI FILAMU
Sunday, November 7, 2010
JUMAPILI YA MARAFIKI!
Thursday, October 28, 2010
HAYA WADAU MPANGO UKO HIVI!

Picha mbili zinazoonyesha matangazo ya wanamuziki wawili na ziara zao jijini paris, tayari washabiki wa damu wa muziki wa Congo wameanza kutupa maoni yao juu ya ushindani usoisha wa wakali hawa wa Congo wakiufananisha upinzani wao na ule wa jb mpiana na werrason, haya mdau nimerudi mzigoni kaa nami ujue nini kitatokea huko paris wakati hapa bongo sie mwezi ujao tutamwona live fally ipupa kwa mara ya pili kama mwanamuziki wa kujitegemea.
Monday, October 25, 2010
FERRE NA FALLY VITA MPYA UFARANSA!


katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni mwendelezo wa vita ya kimuziki kati yao wanamuziki matata wa congo FALLY IPUPA na FERRE GOLA wanatarajiwa kuwa katika vita ya kufungua mwaka jijini paris, wakati fally anadai ziara yake ilipangwa na kutangazwa mapema waratib wa ziara ya ferre wameingilia mpango huo na kutaka kutibua hali ya hewa kwa wapenzi wa muziki huo waliojaa nchini ufaransa.
Wednesday, June 9, 2010
ITS BIG DAY FOR BIG JOE!
Saturday, March 27, 2010
NIMEWAMIS MNO NDUGU ZANGU!
wajameni awali ya yote niombe radhi kuwa siku za hivi karibuni blogu yenu pendwa imekuwa na kwikwi mara kwa mara, hii ni kutokana na sababu zilizo nje kabisa ya uwezo wangu, lakini yote ni majaaliwa yake jalali, inshallah yatakwisha na hali itarejea kama hapo kabla, kwa sasa naomba niwasalimu tu kwani nagonjeka, afya imeleta mgogoro kidogo, tuvute subra nitarejea kumwaga uhondo kwenu wadau.
Subscribe to:
Posts (Atom)















